Hofu kwa wafanyabiashara kuhusu muswada wa fedha 2024 nchini Kenya
Manage episode 420959628 series 1226838
Msikilizaji kwa wiki kadhaa sasa nchini Kenya, kumekuwa na mjadala mkali baada ya kutolewa kwa mapendekezo ya serikali kuhusu muswada wa fedha wa mwaka 2024 unaolenga kuongeza kodi katika baadhi ya sekta na bidhaa nchini humo.
Wazalishaji na wawekezaji wakitarajiwa kuwa waathiriwa wakbwa ikiwa muswada huu utapitishwa kama ulivyo, ambapo baadhi ya vinavyolalamikiwa na wazalishaji ni nyongeza ya ushuru wa thamani katika malighafi kutoka nje pamoja na tozo za mazingira maarufu kama Eco Levy.
Sekta ya uzalishaji wa viwanda inatarajiwa kuchangia asililia 20 katika pato ghafi la taifa hadi kufikia mwaka 2030.
Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, imezungumza na mwenyekiti wa shirikisho la wazalishaji nchini Kenya, Antony Mwangi, kuangazia changamoto na faida za muswada huu.
Jina langu ni Emmanuel Makundi, karibu.
Msikilizaji nilianza kwa kumuuliza Antony, wao wanautazamaje muswada huu?
Insert ///
Msikilizaji kama umeungana nasi Makala ni Gurudumu la uchumi na leo tunaujadili muswada wa fedha nchini Kenya unaoelnga kuongeza ushuru wa bidhaa na wazalishaji, na tunazungumza na Antony Mwangi, mwenyekiti wa shirikisho la wazalishaji nchini Kenya.
Insert ///
Kufikia hapa ndio tunatia nanga ya Makala ya Gurudumu la uchumi kwa juma hili, shukrani kwa Antony Mwangi, mwenyekiti wa shirikishi la wazalishaji nchini Kenya, usikose kuungana nami katika makala nyingine wiki ijayo, ulikuwa nami Emmanuel Makundi, kwaheri.
24 епізодів