Content provided by France Médias Monde and RFI Kiswahili. All podcast content including episodes, graphics, and podcast descriptions are uploaded and provided directly by France Médias Monde and RFI Kiswahili or their podcast platform partner. If you believe someone is using your copyrighted work without your permission, you can follow the process outlined here https://player.fm/legal.
Player FM - Podcast App Go offline with the Player FM app!
Was she the victim of foul play, an accident, or did she choose to disappear? In this episode of The Vanished, we retrace Diana’s last known movements, strange witness accounts, and the lingering mystery that has never been solved or.. was never meant to be solved.
Content provided by France Médias Monde and RFI Kiswahili. All podcast content including episodes, graphics, and podcast descriptions are uploaded and provided directly by France Médias Monde and RFI Kiswahili or their podcast platform partner. If you believe someone is using your copyrighted work without your permission, you can follow the process outlined here https://player.fm/legal.
Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.
Content provided by France Médias Monde and RFI Kiswahili. All podcast content including episodes, graphics, and podcast descriptions are uploaded and provided directly by France Médias Monde and RFI Kiswahili or their podcast platform partner. If you believe someone is using your copyrighted work without your permission, you can follow the process outlined here https://player.fm/legal.
Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.
Taka za kieletroniki zinajumuisha vitu vingi ambavyo ni hatari kwa afya ya binadamu na mazingira na utupaji ovyo ni chanzo kikuu cha madhara, dutu hizi hatari zikiwa na uwezo wa kuchafua udongo, maji, hewa na vyanzo vya chakula. Shirika la E-Waste Initiative Kenya linatoa suluhu ya taka za kieletroniki. Bonyeza hapa kufahamu zaidi.…
Mkaa wa Briketi hutengenezwa kutoka kwa vumbi la mkaa wa kawaida, taka za kilimo au mabaki ya mbao, na hutumiwa kimsingi kwa mapishi nyumbani, shuleni na hata katika makampuni. Mkaa huu una faida kwa kuwa unapunguza uchafuzi wa mazingira, kupunguza ukataji wa miti lakini pia huwaka kwa muda mrefu na kwa usawa zaidi kuliko mkaa wa kawaida, na kuufanya kuwa chaguo maarufu kwa kupikia.…
Makala haya yanazungumzia jinsi Wakulima wengi nchini Kenya wanakumbatia mbinu mpya za kudhibiti wadudu waharibifu wa mimea kwa kutumia madawa ya kiasili badala ya kemikali za viwandani. Kutokana na madhara yanayotokana na matumizi ya dawa za kemikali,wakulima hawa sasa wanageukia madawa hayo asilia kuimarisha mazao na mazingira , Mimea kama vile ,pareto,kitunguu saumu,pilipili na hata mtunguja pori yaani sodom apple sasa inatumika kutengeneza madawa hayo.…
Utunzaji wa bustani ya nyumbani, ni mbinu mpya ya kilimo inayolenga kutimiza malengo matatu kwa wakati mmoja: kuongeza mapato ya kilimo, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuimarisha ustahimilivu, halkadhalika kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi. Bustani ya Nyumbani, kwa kawaida huwa karibu na jikoni au pia kwenye roshani. Bustani hii ambayo mara nyingi hutumia mbolea asilia husaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu na pia kutunza udongo. Bustani hii hutumika kwa kilimo cha mboga, viungo vya upishi kama vitunguu, matunda, au mimea ya kitiba kwa matumizi.…
Rais Donald Trump kwa mara nyingine alitangaza Marekani kujiondoa kwenye Mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, hatua ambayo imeibua mjadala wa kimataifa. Tangazo hilo lilikuja huku ulimwengu ukishuhudia viwango vya joto vinavyovunja rekodi na majanga yanayozidi kuwa makali yanayohusiana na hali ya hewa. Lakini wadadisi wa mambo na viongozi wengine wa ulimwengu wanatazamaje hatua yake Trump? Bonyeza usikilize zaidi.…
Sekta ya mitumba inauwezo wa kuchangia mabilioni ya fedha katika mapato ya taifa, pamoja na kutoa maelfu ya ajira katika mataifa ya bara Afrika na ulaya. Kulinga na utafiti wa Oxford Econimics mwaka uliopita; 2024, sekta ya mitumba pekee ina dhamani ya dola bilioni 8 na imetoa ajiri ya idadi ya zaidi laki moja na elfu 60 kwa vijana nchini Msumbiji , Ghana na Kenya . Lakini hata hivyo wanaharakati wa mazingira wanasema baadhi ya nguo hizo za mitumba zinazoletwa Afrika zinachangia katika uchafuzi wa mazingira. Hili kufahamu Zaidi mwandishi wetu George Ajowi alizuru soko la Gikomba na kutuandalia makala yafuatayo .…
Matumizi ya kuni yanaweza kuwa na athari chanya na hasi kwa mazingira, kulingana na jinsi zinavyovunwa, kutumiwa na kusimamiwa. Leo mwandishi Christopher Karenzi kutoka Kigali, Rwanda ameangazia hatua ya kuondokana na matumizi yake lakini changamoto pia raia wanazokumbana nazo.
Mashirika kadhaa ya kilimo pamoja na serikali ya Kenya yaliwakutanisha wadau wa kilimo—wakulima, wataalamu wa mabadiliko ya tabianchi, na watunga sera—jijini Nairobi mwezi Novemba mwaka uliopita. Mkutano huo ukilenga kuweka bayana mwelekeo wa kutumia kilimo kinachokabili mabadiliko ya tabianchi yaani climate smart agriculture ili kuongeza uzalishaji wa chakula.Hii leo katika makala mazingira leo dunia yako Kesho ,tunaangania kilimo hicho…
Tunaangazia ikiwa tunaweza kuwa na mazingira tulivu bila kelele chafuzi katika maeneo tunayoishi lakini pia sehemu tunazofanya kazi. Tunaangazia ikiwa tunaweza kuwa na mazingira tulivu bila kelele chafuzi katika maeneo tunayoishi lakini pia sehemu tunazofanya kazi.
Makala haya yanazungumzia jinsi dampo la Taka la Nkumba nchini Uganda limekuwa tishio la kimazingira kwa ziwa victoria ambalo ndilo chanzo kuu cha mto Nile.Baada ya dampo la Kiteezi jijini Uganda kuporomoka Agosti 9 mwaka wa 2024 na kuwauwa watu kadhaa,serikali nchini humo ilitoa amri taka zote kutoka Kampala ielekezwe Nkumba karibu na ziwa ,hatua hiyo ikiongeza uchafuzi zaidi wa mazingira .…
Katika miji ya pwani ya Kenya, vita dhidi ya uraibu vimepata mwelekeo mpya wa kusisimua. Kupitia miradi ya kimazingira, vijana kutoka vituo vya kuwarekebisha tabia hawajizuia tu na mihadarati, bali wanabadili jamii zao pia kupitia miradi hiyo. Mwanahabari wetu Victor Moturi alitembelea Mtopanga, Kaunti ya Mombasa, ambako vijana wamepata matumaini kutokana na utunzaji wa mazingira huku wakipata riziki.…
Mkutano wa kukabiliana na uchafuzi wa plastiki ulikamilika mwanzoni mwa Disemba 2024 bila mwafaka kufikiwa, wataalam wa mazingira wakisema pendekezo la kuchakata plastiki wakati nchi nyingine zikiendelea kuzalisha sio suluhu la tatizo hilo. Kwenye makala hii leo tunaangazia athari za plastiki kwa afya na mazingira, suluhu zinazopendekezwa lakini pia kupata ufafanuzi zaidi kilichokwamisha kupatikana kwa mkataba wa kumaliza tatizo linalosababishwa na uchafuzi wa plastiki.…
Mkutano wa hali ya hewa COP29 ukiendelea nchini Azerbaijan, masuala yanayoibua changamoto ni ufadhili, mchakato wa kuondokana na mafuta kisukuku, athari ambazo zimekumba bara la Afrika kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, kuongezeka kwa viwango vya joto lakini pia suluhu zinazopendekezwa na wataalam wa mazingira. Kauli mbiu ya mwaka huu kwenye mkutano wa COP29 ni uwajibikaji wa ufadhili haswa kutoka mataifa tajiri ambao wanachangia kwa viwango vikubwa uchafuzi wa mazingira wakati athari zake zinaathiri nchi zisizojiweza na shirika la mazingira la Greenpeace Africa linapendekeza mustakabali wa nishati mbadala na haki ya hali ya hewa kwa Afrika. Kwa mengi zaidi bonyeza ili kusikiliza makala.…
Player FM is scanning the web for high-quality podcasts for you to enjoy right now. It's the best podcast app and works on Android, iPhone, and the web. Signup to sync subscriptions across devices.